NGARA, KAGERA: AMUUA MWANAYE KWA KUMCHOMA MOTO MAKALIONI NA USONI - Mkazi wa Kijiji cha Kazingati, Kata ya Keza anashikiliwa na Jeshi la Polisi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mwanaye wa miaka miwili - Juma Daniel anatuhumiwa kwa kumchoma moto usoni na makalioni mtoto wake, na kumjeruhi sehemu za haja kubwa kwa kifaa cha ncha kali. Inaelezwa kuwa, baba huyo alifanya hivyo baada ya mtoto kujisaidia haja kubwa kitandani wakiwa wamelala - Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema tukio hilo lilitokea Desemba 27 mwaka jana na mtoto huyo hakupelekwa hospitali. Daniel alimtibu kienyeji nyumbani na baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, alitoroka

Comments