JE, NI KWELI HAKUNA UTAJIRI WA HALALI? - Mdau wa JamiiForums anadai ili uweze kuwa tajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya huruma, utu, wema na ushikamane na Ulimwengu wa giza, dhuluma na uwe katili japo kwa kificho - Anadai, itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi, uuze kwa faida kubwa. Uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako - Lakini pia mdau anaeleza kuwa itabidi ununue hata kuuza mali za wizi au magendo ili usitetereke kiuchumi. Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi. Ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri - Aidha, Mdau anadai ukiwa tajiri, kwa kiunafiki na kuficha makucha yako utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii - Je, una maoni gani kwenye hoja hii ya mdau?
Comments
Post a Comment