GEITA: BABA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MTOTO WAKE WA KAMBO
-
Jeshi la Polisi wilayani Chato limemfikisha Mahakamani, Kazimili Dotto akituhumiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kambo, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili
-
Mwendesha Mashtaka Mauzi Lyawatwa, amesema kosa la ubakaji ni kinyume na Vifungu vya 130(1)(2)(e) na 131(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai
-
Februari 17, 2020 Mshtakiwa akiwa nyumbani kwake, alimwita mtoto huyo na kumwomba amletee maji ya kunywa ndani ya chumba anacholala na mkewe kabla ya kumbaka na kumlawiti
-
Inadaiwa baada ya mtoto huyo kufikisha maji, alikamatwa kwa nguvu na kutupiwa kitandani na baba yake ambaye alimvua nguo za ndani na kuanza kumbaka na kumlawiti
-
Inaelezwa kuwa Mama wa mtoto alikuwa shambani na aliporejea, alisukuma mlango wa chumba chake uliokuwa umeegeshwa, kisha kumkuta mumewe akitenda unyama huo
-
Baada ya kutolewa maelezo hayo na Upande wa Jamhuri, Mshitakiwa alikana kuhusika na mashtaka yanayomkabili. Hakimu Mkazi Mfawidhi Odira Amworo, aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 24 mwaka huu

Comments