LIBYA: MJUMBE WA UMOJA WA MATAIFA AJIUZULU

LIBYA: MJUMBE WA UMOJA WA MATAIFA AJIUZULU
-
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Libya, Ghassan Salame, amejiuzulu baada ya kudumu katika nafasi hiyo kwa takriban miaka mitatu
-
Salame ambaye ni Waziri wa Zamani wa Utamaduni wa Lebanon amesema anajiuzulu kutokana na sababu za kiafya. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameandika hawezi tena kubaki katika nafasi hiyo kutokana na msongo wa mawazo
-
Aliteuliwa na UN mwaka 2017 katika jitihada za kumaliza machafuko nchini Libya baada ya aliyekuwa Rais kwa miaka 40, Marehemu Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani
-
Kabla ya kujiuzulu, Salame amewahi kulalamika mara kadhaa kuhusu kukosa ushirikiano kutoka kwa mataifa ya nje ambayo yanaunga mkono moja kati ya Serikali mbili zilizopo Libya
-
Libya ambayo ina utajiri mkubwa wa mafuta iliingia katika machafuko baada ya kupinduliwa kwa Gaddafi mwaka 2011 na kupelekea nchi hiyo kuwa na Serikali mbili pinzani

Comments